Liverpool Kuchukua Hatua Haraka
Liverpool wapo tayari kuingia mkataba mpya na kinda wao machachari, Rio Ngumoha, baada ya klabu ya Bayern Munich kujitokeza na kutaka saini ya mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea. Ngumoha alikuwa mmoja wa wachezaji walioteka hisia za mashabiki wa Liverpool msimu wa 2025/26 kutokana na kiwango chake bora, licha ya klabu hiyo kupitia kipindi kigumu.
Kila alipopata nafasi ya kuingia uwanjani, Ngumoha alionyesha soka la kiwango cha juu. Hata hivyo, wengi walihisi kuwa alistahili kupata nafasi nyingi zaidi kuliko alizopewa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Arne Slot. Kwa sasa, kuteuliwa kwa kocha mpya Andoni Iraola kunatajwa kuwa fursa nzuri kwa Ngumoha kujiimarisha zaidi kikosini, ingawa bado anatajwa sana kwenye rada za miamba ya soka ya Ujerumani, Bayern Munich.
Bayern Munich Wagonga Hodi
Bayern Munich wapo sokoni wakitafuta winga wa kushoto wa kuleta ushindani kwa Luis Diaz, na wameamua kuelekeza nguvu zao kwa Ngumoha baada ya kukosa saini ya winga mpya wa FC Barcelona, Anthony Gordon.
Mapema mwezi huu, ripoti za kushangaza zilidai kuwa Ngumoha alikuwa amefikia makubaliano ya mdomo na Bayern Munich kabla ya dili hilo kukwama, lakini mabingwa hao wa zamani wa Ujerumani bado wanaendelea kufuatilia nyendo zake. Hivi karibuni, ripoti nyingine zimebainisha kuwa Bayern wamegonga tena hodi Anfield wakimuhitaji kijana huyo kama lengo lao kuu la usajili, ingawa Liverpool wamekataa katakata madai ya mchezaji huyo kuondoka.
Mipango ya Liverpool na Hasira za FSG
Mwandishi wa habari za michezo, Pete O\u2019Rourke wa Football Insider, ameripoti kuwa Liverpool wanataka kukamilisha mkataba mpya na Ngumoha mara tu atakapotimiza umri wa miaka 18 mwishoni mwa mwezi Agosti. Inadaiwa kuwa wamiliki wa Liverpool (FSG) hawakufurahishwa kabisa na taarifa za Bayern kuingilia kati na kujaribu kumshawishi mchezaji wao.
Katika mahojiano na Football Insider, O\u2019Rourke alisema:
"Ni wazi kuwa Liverpool hawana mpango kabisa wa kumpoteza Rio Ngumoha hivi karibuni. Anaonekana kama nyota mkubwa wa baadaye wa klabu hiyo ya Anfield. Ana mkataba hadi mwaka 2028, lakini nadhani viongozi wa Liverpool watakuwa na shauku kubwa ya kukaa chini na wawakilishi wa Ngumoha ili kukubaliana mkataba mpya atakapotimiza umri wa miaka 18 baada ya miezi michache."
"Liverpool hawajafurahishwa na taarifa kuwa Bayern Munich wamefikia makubaliano binafsi na mchezaji huyo katika jitihada za kukamilisha usajili wake."
Kurithi Mikoba ya Mohamed Salah
Ngumoha anatajwa kuwa mchezaji anayejiamini na mwenye uwezo wa kuziba pengo lililoachwa na Mohamed Salah klabuni hapo. Hata hivyo, kuna madai kuwa Salah angebaki kikosini humo kama angejua mapema kuwa Arne Slot angeondoka.
Kiungo wa zamani wa Liverpool, Danny Murphy, ametoa mtazamo wake akieleza kwa nini haamini kama uamuzi wa Salah ungekuwa tofauti. Akizungumza na GOAL, Murphy alisema:
"Nadhani kitu kikubwa kilichoathiri uamuzi wake wa kuondoka ni kiwango chake cha uwanjani. Kuna uwezekano mkubwa kwamba kama ungekuwa na uhusiano mzuri na kocha, labda ungebaki na kujaribu kurejesha kiwango chako msimu unaofuata."
"Nadhani anahisi\u2014kama wachezaji wengi wanavyohisi wanapofikia hatua hiyo\u2014kwamba huwezi kufikia tena kile kiwango cha juu ulichokuwa nacho zamani, hivyo ni bora kuondoka kabla mambo hayajazidi kuwa mabaya."
Murphy aliongeza kuwa lawama zote haziwezi kutupwa kwa aliyekuwa kocha wao:
"Suala la Slot lipo hapo, na tutakuwa wajinga kama tutakataa hilo. Kuna nafasi ndogo, lakini sina hakika kama kuna kocha yeyote ambaye asingelazimika kumweka benchi kutokana na jinsi alivyokuwa akihangaika uwanjani. Kama kuna lolote, naona Slot alimvumilia kwa muda mrefu sana uwanjani. Mashabiki walikuwa wakitaka apumzishwe, lakini kocha alimwacha acheze kwa kipindi kirefu zaidi ya ambavyo makocha wengi wangefanya. Kwa hiyo, nadhani matatizo hayo yangejitokeza tu hata kama angekuwa na uhusiano mzuri na kocha yeyote yule."
Kwa sasa, Liverpool wamejipanga kuhakikisha wanalinda hazina yao ya baadaye kwa kumpa Rio Ngumoha mkataba mpya utakaomfanya asahau kabisa ofa za Bayern Munich na kelekeza nguvu zake chini ya kocha mpya Andoni Iraola.